Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga wanaokabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya.
Wakili wa Sugu, Peter Kibatala ameongea na AyoTV na millardayo.com na kuelezea ilivyokuwa Mahakamani na pia amegusia kilichokuwa kinakwamisha Sugu kupata dhamana toka afikishwe Mahakamani January 2, 2018.
ALICHOZUNGUMZA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KESI YAKE NA HAMISA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA