Staa wa soka wa Tanzania anayecheza katika klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji Mbwana Ally Samatta usiku wa February 10, 2018 aliingia uwanjani kucheza mechi yake tano toka apone maumivu ya mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia.
Dakika ya 36 ya game aliumia tena kwenye mchezo wa jana wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Zulte-Waregem kwenye mchezo wa ligi kuu nchini humo na nafasi yake kuchukuliwa na N’Dongala.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare 1-1. Kipindi cha pili Genk ilipata mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Thomas Buffel DK. 59 na kiungo Alejandro Pozuelo DK. 90 na kuifanya Genk kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1.
Mkemi kuhusu kauli ya Manara “Sisi mpango wa kuishangilia Simba hatuna”