Kutoka nchini Kenya nakusogezea taarifa inayohusu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga kilichopo Bondo asubuhi ya leo February 10, 2018 wameanzisha vurugu kufuatia kifo cha mwenzao aliyekuwa klabu ya usiku siku ya Ijumaa jioni.
Wakati wa maandamano na vurugu hizo, wanafunzi hao wamechoma moto klabu ya usiku, ambapo mwenzao huyo alichomwa kisu hadi kupoteza maisha na kufanya shughuli zote za eneo hilo ikiwa ni pamoja na shughuli za biashara katika eneo hilo la Bondo kusimama.
Kifo cha kijana huyo kilitokea baada ya ugomvi kutokea ukimuhusisha marehemu huyo na wenzie kuhusu mwanamke jambo lililofanya mabaunsa wa klabu hiyo kuingilia kati, hadi kijana huyo kuchomwa kisu. Alipelekwa hospitali lakini alipoteza maisha pindi tu alipofika.
TATU MZUKA: Kitu amefanya Mshindi wa Mil 22 baada ya Kuipokea pesa fake
Mwenyekiti UVCCM Arusha amepanga kuwashtaki Wabunge wa Arusha