Taarifa niliyopokea kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo February 10, 2018 amempandisha cheo na kumteua Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema kuwa Rais Magufuli amempandisha cheo Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo February 10, 2018.
Kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.
Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.
ALICHOZUNGUMZA KIBATALA BAADA YA SUGU KUACHIWA, AMETAJA KILICHOKUWA KINAKWAMISHA DHAMANA