Leo February 10, 2018 stori kubwa inayoshika headlines Afrika Kusini ni kumhusu Mwenyekiti wa chama tawala nchini humo hii leo amejaribu kutuliza shauku ya kitaifa kuhusiana na hatima ya rais Jacob Zuma na kusema taifa hilo linapaswa kuwa na uvumilivu na kusubiri hatima ya mazungumzo ya siri yanayoendelea kuhusiana na uwezekano wa kiongozi huyo kujiuzulu.
Rais Jacob Zuma anakabiliwa na shinikizo kubwa akitakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi na katika siku za hivi karibuni amekuwa akiendelea na mazungumzo juu ya haja ya kukabidhi madaraka kwa Cyril Ramaphosa ambaye ni Makamu wake.
Gwede Mantashe ambaye ni mwenyekiti kitaifa wa chama cha African National Congress amesema katika mkutano wa chama hicho kuwa Ramaphosa anapaswa kupewa muda kumaliza majadiliano yanayoendelea. Ramaphosa anatarajia kutoa hotuba hapo kesho Jumapili katika maadhimisho ya miaka 28 tangu Rais wa kwanza muafarika nchini humo Hayati Nelson Mandela atoke jela.
Tazama Fundi nguo asiyeona akishona, “Nashona mpaka saa 6 usiku na siwashi Taa”