Moto ulizuka katika hospitali ya Mission ya Tenweek na kusababisha wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo kulazimika kukimbia wodi ili kuokoa maisha yao baada ya moto huo kuteketeza baadhi ya majengo
Hospitali ya Tenweek ipo katika Jimbo Bomet nchini Kenya, ilishika moto baada ya jiko la hospitali hiyo kulipuka na kuteketeza maeneo ya karibu ikiwemo store ya chakula na mgahawa na baadhi ya vyumba ambayo viko karibu na kitengo cha waonjwa mahututi na wodi kuu.
Mkuu wa Polisi Jimbo la Bomet, Samson Rukunga amesema jeshi la polisi limejitahidi kudhibiti moto huo usiathri sehemu kubwa na kuwahi kuuzima na hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu.