Jana mashabiki wa Man United wali-post picha tofauti za Adnan Januzaj wakimtakia happy birthday, lakini leo wata-post picha za Munich air disaster iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1958.
Tarehe 6 February mwaka 1958 huko Munich kwenye Munich-Riem Airport ndege ya British European Airways safari namba 609 ilipata ajali baada ya jaribio la tatu kutakaa kupaa.
Kwenye hiyo ndege kulikuwa na wachezaji wa Manchester United,mashabiki na waandishi wa habari.Watu 23 kati ya 44 walifariki baada ya ajali hiyo na wengine walijeruhiwa.
Kama umezaliwa leo basi unasherekea siku yako ya kuzaliwa na gwiji la muziki wa reggae Bob Marley ambaye alifariki akiwa na miaka 36 na alizaliwa 6/2/1945.
“Money can’t buy life”, unaambiwa hayo ni maneno ya mwisho ambayo Bob alimwambia mwanae Ziggy kabla mauti hayajamkuta.
Licha ya kufariki muda mrefu kidogo, mwaka 2001 iliwekwa nyota ya Bob Marley kwenye Hollywood Walk of Fame. Mwaka huo huo pia alitunukiwa Grammy Lifetime Achievement Award na BBC wakautaja wimbo wa One Love kama song of the millennium.
Historia ya logo ya viatu vya Jordan ilianza tarehe kama ya leo mwaka 1988 ambapo Michael Jordan alifunga kikapu kwa slam dunk huku akitengeneza logo maarufu ya kwenye viatu vyake.
Kama ulikua hujui ile logo ya Jordan haikuchorwa tu, bali Michael Jordan mwenyewe akiwa kwenye mashindano ya dunk competition aliluka kama logo ilivyo na mchoro ukaanzia hapo