Kutoka Uingereza moja kati ya habari kubwa leo February 12, 2018 ni kufungwa kwa dharura kwa Uwanja wa Ndege wa ‘London City’ huku safari zote zikifutwa hadi taarifa zaidi zitakapotolewa na mamlaka husika.
Kufungwa kwa uwanja huo wa ndege kunatokana na kupatikana kwa bomu la Vita ya Kwanza ya Dunia katika eneo la karibu na eneo lijulikanalo kama Mto Thames katika eneo la uwanja huo wa ndege.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Jeshi la Polisi Jijini humo tayari wameanza kushughulikia suala hilo ili kuliondoa bomu hilo.
Kwa leo tu, uwanja huo wa ndege ulikuwa unatakiwa kuhudumia wasafiri 16, 000 lakini wameambiwa wawasiliane na makampuni ya ndege walizokuwa wanasafiri nazo.
Wafanyakazi 800 wapunguzwa kazini, Mkurugenzi atuma ombi kwa JPM
Ni kweli AY kafunga ndoa ya siri Rwanda?