Leo February 12,2018 Upande wa mashtaka umebainisha kuwa upelelezi wa kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo na Mkurugenzi wa PALMS Foundation, Wayne Lotter inayowakabili watu watatu akiwemo Meneja wa Benki, Khalid Mwinyi haujakamilika.
Mbali ya Mwinyi, watuhumiwa wengine ni mfanyabiashara Rahma Almas (Baby) na Mohammed Maganga ambaye ni mchimba makaburi.
Wakili wa serikali Saada Mohamed amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.
Hata hivyo, mshtakiwa Almas aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa Maganga ambaye ni mchimba makaburi anaumwa.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi February 21, 2018 kwaajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande
Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na kosa la mauaji ambapo wanadaiwa walitenda kosa hilo August 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selasie Kinondoni DSM, ambapo walimuua Wayne Lotter.
ALICHOZUNGUMZA KIBATALA BAADA YA SUGU KUACHIWA, AMETAJA KILICHOKUWA KINAKWAMISHA DHAMANA