Mwanamke mmoja kutoka nchini Ufaransa Cecile Bourgeon mwaka 2013 alidai kwamba binti yake mwenye umri wa miaka mitano Fiona alikuwa amepotea katika Hifadhi ya Clermont-Ferrand wakati akicheza na mdogo wake wa kike wa miaka 2.
Jambo hilo lilizua hisia mbalimbali nchini humo lakini baada ya miezi minne ya kumtafuta mtoto huyo, Cecile na mpenzi wake Berkane Marklouf walikiri kumzika mtoto huyo msituni baada ya kutokea ajali nyumbani na mtoto huyo kufariki.
Mwanamke huyo alihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kudanganya kuhusu kupotea kwa mwanaye mwaka 2016. Hatahivyo rufaa iliyokatwa siku za hivi karibuni na kusimamiwa na jopo la Wanawake Mawakili 9 imemhukumu mwanamke huyo miaka 20 jela ikiwa ni mara nne zaidi ya kifungo cha kwanza.
Hekari 8 za Bangi za fyekwa tena Arusha, Viongozi watatu wa Serikali wanatafutwa
RC Mongella na Kamati ya Ulinzi na Usalama walivyofanya kazi ya kupasua na kubeba Mawe