President John Magufuli leo February 12, 2018 amepokea taarifa kutoka kwa viongozi wa Shirika la Simu Tanzania kuhusu mwelekeo wa shirika hilo baada ya kuanza kutumika kwa sheria namba 12 ya mwaka 2017 ya Shirika la Simu Tanzania, iliyolibadili kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kuwa Shirika la Simu Tanzania (TTCL Corporation).
Pamoja na kupokea taarifa hiyo JPM amemteua Dkt. Omari Rashid Nundu kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Corp na Waziri Waziri Kindamba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corp, amewataka kuchapa kazi kwa juhudi na kuhakikisha TTCL Corp inaongeza ufanisi, na kutoa gawio kwa Serikali.
Dkt. Omari Rashid Nundu na Waziri Waziri Kindamba wamemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi huo na wamesema TTCL itaendelea kujiimarisha kwa kupanua huduma za mawasiliano nchini, kuongeza na kuboresha bidhaa ikiwemo TTCL Pesa, kuzalisha faida zaidi na kuusimamia vizuri mkongo wa Taifa kwa maslahi na usalama wa nchi.
WAFANYAKAZI 800 WAPUNGUZWA KAZINI, MKURUGENZI ATUMA OMBI KWA JPM