Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqaro ameagiza Baraza la Halmashauri ya jiji la Arusha kutekeleza agizo alilolitoa la halmashauri kutenga Tshs Bilioni 3 kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo kwa ajili ya sekta ya elimu.
Ameeleza kuwa lengo kuu ni kusaidia Elimu bure na kutatua changamoto za elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa na kumaliza kabisa tatizo la miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari, ikiwa ni pamoja na madarasa, nyumba za walimu, vyoo na uzio wa shule hizo.
DC Daqaro ameainisha kuwa suala hilo linawezekana kwani Halmashauri inakusanya zaidi ya Tshs Bilioni 14 na baraza kutenga Milioni 700 kwa ajili ya elimu ni kiasi ambacho ni kidogo sana ukilinganisha na mwitikio mkubwa wa wazazi kusomesha watoto wao katika shule za serikali.
Baada ya Wizara ya AFYA kuhamia Dodoma, Jengo lao wamepewa wengine?
Utafiti wa mapato na matumzi binafsi utafanyika katika kaya 408 Mwanza.