Kutoka nchini Marekani katika Jimbo la Florida zaidi ya watu 17 wanaripotiwa kufariki dunia, 15 wakiwa wanafunzi na wengine kujeruhiwa baada ya shambulio la risasi lililofanyika katika eneo la shule ya Marjory Stoneman Douglas High School iliyopo Parkland lililofanywa na kijana wa miaka 19, February 14, 2018.
Kijana huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nikolas Cruz alikuwa ni mwanafunzi katika shule hiyo lakini inaelezwa kuwa alifukuzwa. Alitumia silaha aina ya AR-15-riffle, magazine, pamoja na mabomu ya mkono kutekeleza tukio hilo.
Maaskari wa eneo hilo wameeleza kuwa kabla ya kuanza kushambulia katika eneo hilo, Nikolas aliwasha kengele ya tahadhari ya moto ili kufanya wanafunzi watoke nje na walivyotoka akaanza mashambulizi.
Kijana huyu alifukuzwa shule kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu na tayari amekwisha kamatwa na mahojiano yanaendelea.
Inaripotiwa kuwa eneo hilo limejaa watu, familia mbalimbali za watoto wanaosoma shule hiyo zimefurika kufahamu usalama wa watoto wao na kuwachukua na kutambua miili iliyokufa kama ni ya watoto wao.
Alichozungumza Riyama Ally na Mume wake kuhusu siku ya Valentines Day
CONFIRMED: Zari ameachana na Diamond Platnumz