Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Lameck Nchemba, yupo Mwanza kumnadi mgombea Udiwani Kata ya Isamilo kupitia CCM, pamoja na kumnadi mgombea Waziri Mwigulu amesema tayari amepata taarifa za uhalifu wa watu kupingwa na nondo pamoja na kutekwa kwa madereva bodaboda Mwanza, ameonya na kuziagiza Mamlaka zinazohusika kuchukua hatua dhidi ya huo uhalifu.
“Nimesikia kuna uhalifu wa hapa na pale unatokea hapa, wengine wanateka watu kwenye bodaboda, wanateka watu, niwaambie nimepita hapa Mwanza kufungulia mbwa, wewe endelea kukwapua, hatuwezi kusema ndani ya nchi hii mtu hawezi tembea ikifika Saa moja,” -Dr. Mwigulu
ANGEKUWA ANATOKEA SINGIDA, ANGEIPONGEZA SERIKALI, BAADA YA LISSU KUSHAMBULIWA