Leo February 15, 2018 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage yupo jimboni kwake Wilaya ya Muleba mkoani Kagera ambapo ameamua kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya jimbo lake.
Baada ya ziara yake katika Tarafa tatu Mwijage ameeleza kuwa mpango mkubwa alionao ni kukomboa Wananchi wake kupitia elimu ambapo tayari amejenga shule zake katika Kata mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha wanapunguza wingi wa wanafunzi katika shule moja.
Kupitia jitihada hizo ameeleza kuwa hataki wananchi wake wachangishwe michango kwa nguvu kwa kutumia mgambo badala yake Watendaji waweke utaratibu mzuri wa kuchangia na wakubaliane na wananchi wao, hapo wakigoma bora wapelekewe askari wa FFU.
Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa hataki jimbo lake ndo lizalishe watoto wa kufanya kazi za ndani badala yake Wazazi wawapeleke shule ili baadae waweze kufanya kazi nzuri zitakazowaepusha na kazi za ndani.
Ukarabati uliogharimu Milioni 75 wamfanya Ndalichako kuchukua maamuzi Magumu