Kutoka nchini Kenya, siku chache zilizopita Katibu wa Wizara ya Utalii na Wanyamapori Najib Balala amesifia jambo nchi ya Tanzania katika sekta ya Utalii na jinsi inavyonufaika zaidi kuliko nchi yao.
Balala amezungumzia hali ya Hoteli nchini Kenya na kueleza kuwa kukosekana kwa hoteli za kutosha zenye hadhi nzuri kumefanya Sekta ya Utalii kwenye nchi yao kuwa nyuma ya mafanikio yanayopatikana Tanzania kwa kupokea watalii wengi zaidi Afrika Mashariki.
Ameeleza kuwa japokuwa idadi ya watalii nchini humo imeogezeka kutoka 1,342,899 mwaka 2016 hadi 1,474,671 mwaka 2017, bado miundombinu ya hoteli ya kuvutia Watalii sio bora na kama hali hiyo itabadilishwa sekta hiyo itapokea Watalii zaidi.
“Angekuwa anatokea Singida, angeipongeza Serikali, baada ya LISSU kushambuliwa”
“Nimekuja Mwanza kufungulia mbwa” Waziri Mwigulu