Kutoka nchini Ethiopia, habari zinazoenea kwenye vyombo vya habari vya kimataifa leo February 15, 2018 ni kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hailemariam Desalegn ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri Mkuu.
Ameeleza kuwa tayari amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kama Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Chama Tawala nchini humo, hatahivyo haijabainika iwapo chama hicho kimekubali uamuzi wake au la.
Hailemariam ameeleza sababu ya kujiuzulu kwakwe kuwa ni kusaidia kusuluhisha mzozo wa kisiasa uliopo nchini humo.
Tangazo la Hailemariam linakuja katikati ya mgogoro wa kisiasa na kupinga machafuko katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikiachia huru maelfu ya wafungwa wa kisiasa ili kupunguza mvutano.
Waziri Mkuu amefika Mwanza, kabla ya ziara ameanza na hiki
Ilivyokuwa Kesi ya waliojiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli Nyumbani