Kutoka nchini Hispania, moja kati ya habari zilizozua mjadala kwenye mitandao ya kijamii na kuibua hisia za watu mbalimbali ni kuhusu Kampuni moja ya Mahusiano ya umma na Mawasiliano imeingia matatani baada ya kumnyima binti kazi kwakuwa sio Mwanaume.
Kampuni hiyo iitwayo Impulsa Comunicación ilimwambia binti huyo Carla Forcada mwenye miaka 25 kuwa nafasi hiyo ya kazi inamhitaji Mwanaume kwani yeye hawezi kukimbizana na kasi ya kufanya kazi kwenye makampuni makubwa.
Binti huyo baada ya kuambiwa hivyo na kuondoka ali-post kwenye mitandao ya kijamii juu ya suala hilo, jambo ambalo limepelekea makampuni makubwa kama Cocacola na mengine yaliyokuwa yanafanya kazi na kampuni hiyo kuvunja mkataba nayo.
Uongozi wa kampuni hiyo umeomba radhi na kueleza kuwa hawakuwa na maana ya kumnyanyasa kijinsia binti huyo. Hatahivyo Cocacola kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa umesikitishwa na kitendo kilichofanywa na kampuni hiyo na kueleza kuwa hawawezi kufanya kazi na kampuni yenye sera za upendeleo wa kijinsia.
Waziri Mkuu amefika Mwanza, kabla ya ziara ameanza na hiki
Ilivyokuwa Kesi ya waliojiunganishia Bomba la Mafuta ya Dizeli Nyumbani