Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Dr. Mwigulu Nchemba leo amefanya ziara mkoani Kagera kwa lengo la uzinduzi wa vitambulisho vya Taifa NIDA, ambapo amewasihi Watanzania kuhakikisha wanajiandikisha ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuwakuta hapo baadae.
Akiongea na wananchi Waziri Mwigulu amegusia suala la mauaji ya kada wa CHADEMA ambaye pia alikuwa Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, Daniel John kukutwa amefariki katika eneo la Coco beach Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kufuatia hali hiyo amemuagiza IGP na Vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi haraka sana iwezekanavyo na wahakikishe wanarudisha majibu kwa wananchi, maana watu hawawezi kuuawa na kupotea sisi tukaona kawaida au mazoea.
Aidha amesema kuwa mtu kuwa chama chochote cha siasa haimuondolei ubinadamu wake, kwa sababu hakuna chama chenye thamani kubwa kuliko mtanzania yeyote.