Moja ya habari zilizotufikia hapa Ayo TV na millardayo.com ni kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa uchunguzi huru ufanyike kuhusu kile wanachodai ni matukio ya utekwaji na upotevu wa watu mbalimbali nchini.
Taarifa hii inakuja baada ya kifo cha mjumbe wa chama cha upinzani CHADEMA, Daniel John February 11, 2018 ambaye mwili ulikutwa katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es salaam, siku moja baada ya kutekwa.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Murilo Jumanne Murilo, mwili huo ulikutwa na majeraha ikiwemo shingo yake kukutwa imenyongwa na watu ambao bado hawajajulikana.
Inaelezwa kuwa marehemu pamoja na mwenzake Reginald Mallya aliyenusurika kifo lakini alikutwa akiwa na majeraha mwilini katika maeneo ya mkononi na kichwani.
Agizo la Dr. Mwigulu kwa IGP Sirro kuhusu Kiongozi wa CHADEMA aliyeuwawa