Kutoka nchini Marekani siku za hivi karibuni, Mashirika ya Kiintelijensia (FBI, CIA na NSA) yametangaza onyo kwa raia wa nchi hiyo la kutonunua bidhaa za simu kutoka nchini China.
Wamekataza raia hao kununua simu za kampuni za Huawei na ZTE kwani simu hizo zinahatarisha usalama wa wateja wa simu hizo.
Imeelezwa kuwa serikali ya Marekani haiwezi kuruhusu kila kampuni ya simu ikaingia ndani ya miundombinu ya mawasiliano ya nchi.
Mkurugenzi wa FBI Chris Wray ameeleza kuwa kwa kuachia makampuni hayo ya simu ya Kichina nchini mwao wanakuwa katika hatari ya kupeleleza na kuiba taarifa muhimu za kiintelijensia nchini Marekani.
Nasikia kuna Mabaunsa, Hakuna baunsa mbele ya serikali’- Kamanda Mambosasa