Upelelezi wa kesi ya Uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha wa Shilingi Bilioni 309 inayomkabiki mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na Mfanyabiashara James Rugemarila katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.
Hayo yameelezwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Leornad Swai akishirikiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Swai ameiomba mahakama hiyo iahirishe kesi hiyo hadi tarehe nyingine kwa sababu upelelezi bado haujakamikika.
Kutokana na hoja hiyo, wakili wa utetezi, Michael Ngalo aliiomba mahakama waelezwe upelelezi umefikia wapi ili wajue kipi kinaendelea.
Hata hivyo, Kishenyi ameiomba mahakama kutoruhusu swala la ugonjwa wa washtakiwa kusemwa mahakamani kwani hilo ni suala la kitaaluma zaidi, (Kitabibu).
Amedai, masuala ya ugonjwa ni ya mtu binafsi linapaswa kujadiliwa nje ya Mahakama isipokuwa pale tu mahakama inapotakiwa kutoa amri na si vinginevyo.
“Mahakamani hapa sio mahali sahihi sana pakuleta masuala ya ugonjwa,” – Kishenyi.
Pia kuhusu suala la upelelezi wanalifanyia kazi ili ukamilike.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi March 2, 2018.
Kwa pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh.Bil 309.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Madabida alivyofika Mahakamani katika Kesi yake