Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Ferdnand Wambali amesema mahahakama imekuwa ikitupiwa lawama katika ukamataji mali kwa sababu madalali wengi wa mahakama hawana elimu ya kutosha kuhusu utekelezwaji wa amri hizo.
Kutokana na hali hiyo amemtaka kila mtu anayeomba kufanya kazi ya udalali wa mahakama kuwa na cheti cha umadhubuti katika kazi hiyo toka Chuo cha Uongozi wa Mahakama ama Taasisi inayotambuliwa na kamati ya uteuzi.
Jaji Kiongozi ameyasema hayo leo wakati akifungua kongamano la wadau mbalimbali wa mahakama wanaoratibu na kusimamia utekelezaji wa amri za mahakama wakiwamo madalali.
Kongamano hilo limeratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania lengo ni kujadili rasimu ya mtaala maalum wa kutolea mafunzo kwa watu wanaofanya shughuli za udalali na usambazaji wito na amri za mahakama.
Jaji Wambali amesema mahakama inatambua madalali wa mahakama na wale wanaopaswa kupeleka hati za kutiwa kwenye Mashauri wanawajibu kuhakikisha amri mbalimbali zinazotolewa na mahakama hasa katika Mashauri ya madai zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa.
Kesi ya Rugemarila na Seth ilivyoendelea Mahakamani leo