Stori nayokusogezea ni kutoka Dododma leo February 19, 2018 ni Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili (Mirembe), Tito Onesmo Machibya (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili au la.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama James Karayemaha amesema anahitaji majibu hayo March 5 , 2018 siku ambayo Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani. Agizo hili linakuja likiwa agizo la awali kutotekelezwa.
Machibya ‘Nabii Tito‘ amefikishwa Mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kwa mafundisho anayo yatoa na amekuwa akiieleza Mahakama kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kuonesha vithibitisho kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili.
“KAMA WEWE NI BODABODA, KUNA HAYA YA KUZINGATIA” WAZIRI MKUU