Kwa wapenzi na wateja wa migahawa ya Kentucky Fried Chicken (KFC), habari ambayo inasambaa leo Jumatatu, February 19, 2018 ni kwamba kampuni hiyo imefunga migahawa yake 750 kati ya 900 huko nchini Uingereza.
Inaelezwa kuwa kufungwa kwa migahawa hiyo kunatokana na upungufu mkubwa wa nyama za kuku baada ya kuingia mkataba mpya na kampuni ya usambazaji wa bidhaa DHL na bado haijawekwa wazi kama hali hiyo itarekebishwa hivi karibuni au la.
Msemaji wa migahawa hiyo Uingereza ameeleza kuwa wafanyakazi kwenye migahawa hiyo iliyofungwa wameanza kuambiwa wachukue likizo huku wakisubiri uongozi wa kampuni kushughulikia tatizo hilo.
“Sio wakati muafaka kunyoosheana vidole nani kahusika kumuua Akwilina” -Kigwangalla
Uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli leo February 19