Tarehe kama ya leo mwaka 1958 yaani ( 6 February 1958) – Miaka 62 iliyopita, timu ya soka Manchester united ikiwa na kikosi chenye vijana wastani wa miaka 24 kinachoaminika kuwa imara kuwahi tokea katika historia ya klabu hiyo chini ya kocha Matt busby na kupewa jina la “Busby Babes” kilikuwa kinasafiri kutoka Yugoslavia ambapo walitoka kucheza dhidi ya Red star Belgrade ya nchini humo katika kombe la ulaya yaani ” European Cup”
Ilipofika Ujerumani katika uwanja wa Munich Riem Airport ilibidi watue ili ndege iongezewe mafuta, baada ya hapo katika jaribio la tatu kupaa ndege hiyo ikagonga baadhi ya majengo ikaanguka na kuanza kuwaka moto!
Hii ni video inayoonesha tukio lilivyotokea.
Ndani ya msafara huo kulikuwa na jumla ya watu 44, kati yao kulikuwa na wachezaji, maofisa wa timu, waandishi wa habari na mashabiki ambapo watu 20 hapo hapo walipoteza maisha huku wengine wakikimbizwa katika hospitali ya Recht der Isar ya jijini Munich ambapo dakika chache watu 3 walikufa na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 23 na 21 walinusurika huku kocha mkuu Matt Busby alinusurika akiwa mahututi na kapteni ambaye hadi leo huwa anaonekana katika mechi za Manchester United akiwa kama mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya klabu hiyo Bobby chalton akinusurika salmini!
Katika watu 23 waliokufa kwenye ajali hiyo, wachezaji 8 walikufa hapo hapo na maofisa 3 wa timu, wengine walikuwa mashabiki na waandishi.