Leo February 19, 2018 Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Onanch Timoth ametuletea GoodNews kuwa ifikapo July 2018, vituo vya afya saba katika Mkoa wa Arusha vitakuwa na Huduma ya Upasuaji ili kuepusha mrundikano wa wagonjwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru .
Onanch Timoth ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Huduma hiyo ya Upasuaji iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza katika kituo cha afya Kaloleni ambapo kitakuwa na uwezo wakuhudumia watu zaidi ya wanne.
Nae Doctor Ngeta Semba ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka hospitali ya mkoa amesema ni hatua nzuri kwakuwa wametekeleza agizo la Waziri wa Afya Ummy Mwalimu la kila kituo kuwa na huduma ya upasuaji.
UTEUZI ULIOFANYWA NA RAIS MAGUFULI LEO FEBRUARY 19,