Mbunge wa Jimbo la Ubungo na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika February 19, 2018 amezungumza na AyoTV na millardayo.com akiwa nyumbani kwenye msiba wa Akwilina Maftah.
Mnyika ametoa pole kwa familia ya Akwilina kwa msiba uliotokea na kutaka watu kuacha kuzungumza mambo yasiyohusu msiba kwa sasa pia Mnyika amegusia kuhusu barua waliyoipokea kutoka Jeshi la Polisi ikitaka baadhi ya Viongozi wa Chama hicho kufika ofisi za jeshi la Polisi.
“Nimepewa taarifa kwamba Jeshi la Polisi limepeleka Barua makao makuu ya Chama likituita baadhi ya Viongozi ambao limetutaja kwa majina, wamechelewesha barua makusudi pamoja na kwamba barua imechelewa wameambiwa watutafute popopte tulipo,” -Mnyika
MSIBA WA AKWILINA: MSEMAJI WA FAMILIA KAZUNGUMZA KUHUSU SERIKALI KUGHARAMIA MAZISHI