Nchini Tanzania ni kawaida kuona kesi za mvua zinazosababisha mafuriko ambayo husabisha maafa na uharibifu wa makazi ya watu na mali zao na wakati mwingine watu hupoteza maisha.
Hatahivyo habari kutoka Msumbiji, mvua zilizonyesha siku za hivi karibuni katika Mji wa Maputo zimesababisha rundo la takataka kuanguka na kuwafukia watu 17 ardhini hadi kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa.
Inaelezwa kuwa rundo hilo la takataka ambalo lilikuwa la mita 15 limefunika watu pamoja na nyumba saba.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa Manispaa ya Ka Mavota, Despedida Rita amewaeleza waandishi wa habari kuwa miili 17 tu ndio iliyopatikana, lakini wana wasiwasi kuwa kuna uwezekano ipo miili mingine imefunikwa na hivyo jitihada za kuitafuta zinaendelea.
Kitu cha Kufahamu kutoka Bodi ya Mikopo Tanzania na Jinsi ya Kurudisha
Familia ya AKWILINA kuhusu kugomea kuchukua Mwili hospitali