Leo February 20, 2018 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema wamebaini kuwa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) linaloongozwa na Askofu linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo kinyume na taratibu za utunzaji fedha.
Akiongea na Waandishi wa habari katika Ofisi za Mamlaka hiyo Kichere amesema kumekuwa na utoaji wa kiwango kikubwa cha pesa katika akaunti za benki ambao haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwaajili ya usalama wa fedha na wahusika.
“Tumefanya uchunguzi kuhusu ile kauli kuwa ana pesa kuliko Serikali, tulichobaini kwanza ni kwamba Askofu Kakobe hana fedha wala akaunti katika Taasisi yoyote ya kifedha hapa nchini, ila ni mmoja ya Wasimamizi wa kuu wa akaunti za Kanisa la {FGBF}” -Kichere
“ASKOFU KAKOBE AMEMUOMBA RAIS MAGUFULI MSAMAHA” -TRA