Takribani mwezi mmoja umepita, marubani wawili raia wa Kenya walitekwa na kikundi cha waasi wa nchini Sudani baada ya ndege yao kupata ajali na jitihada za kuwaokoa zilikuwa ziliendelea.
Habari njema leo February 20, 2018 ni kwamba marubani hao wameachiwa na waasi hao na kwa mujibu wa msemaji wa waasi hao marubani hao wameachiwa baada ya kampuni ya bima kulipa zaidi ya dola za Marekani 100,000 sawa na Tsh Milioni 24o za Kitanzania.
Fedha hii ilikuwa niyakulipa fidia ya kifo cha mtu mmoja aliyepoteza maisha baada ya ndege hiyo kupata ajali.
Marubani hao Kapteni Pius Frank Njoroge na Msaidizi wa Rubani Kennedy Shamalla wameripotiwa kuwasili salama mjini Juba na watarudishwa Kenya baadaye.
HEKAHEKA: Mwanaume aelezea jinsi Mkewe alivyopotea na kukuta mwili wake umeliwa
“Askofu Kakobe amemuomba Rais Magufuli msamaha” – TRA