Moja kati ya michezo ya UEFA Champions League ya hatua ya 16 bora msimu wa 2017/2018 iliyokuwa inasubiria kwa hamu ni pamoja na game ya Chelsea dhidi ya FC Barcelona iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.
Chelsea leo alikuwa anaingia katika uwanja wake wa Stamford Bridge akiwa anakumbuka mara ya mwisho kuifunga Barcelona ilikuwa ni April 18 2012 goli 1-0 lililofungwa na Didier Drogba dakika ya 45 ya mchezo, ukiachia ushindi huo game zilizofuatia zote walitoka sare.
Club ya Chelsea ikiwa nyumbani na leo imeendeleza rekodi yake kwa kupata sare yake ya tatu mfululizo dhidi ya Barcelona, baada ya kufungana goli 1-1, goli la Chelsea likifungwa na Willian dakika ya 62 huku la Barcelona likifungwa na Lionel Messi dakika ya 75, hivyo Chelsea ana kazi ya kwenda kupindua game ya marudiano Nou Camp kwani ni lazima apate ushindi au sare ya kuanzia magoli mawili.
Naambiwa haya ndio magari ya Mbwana Samatta anayotumia Ubelgiji