Leo February 21, 2018 Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Musa Matoroka amewapokea madiwani Prosper Msofe na Obed Meng’oriki wa CHADEMA ambao wametangaza kujivua uanachama.
Prosper Msofe ambaye alikuwa Diwani wa Kata ya Daraja Mbili alijivua uanachama wa CHADEMA jana huku Obed Meng’oriki akijivua uanachama wa chama hicho leo na wote wawili wameshapokelewa rasmi CCM.
Wawili hao wameeleza kuwa wameamua kujiunga na CCM kwa madai kuwa wanataka kuunga mkono jitihada za uongozi wa Rais John Magufuli.
Matoroka ametoa ujumbe kwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuwa wamejiandaa kuchukua jimbo hilo hivyo aanze kutafuta kazi nyingine.
Diwani wa CHADEMA aliyewekwa ndani na Meya wa CHADEMA kahamia CCM
DC Madusa aagiza Polisi kukamata Wanaojiuza, kuvaa Vimini na Milegezo ili wakafyatue Tofali