Kutoka nchini Syria, leo February 21, 2018 taarifa zilizoenea ni kwamba watu zaidi ya 250 wameuawa katika saa 48 zilizopita kutokana na mashambulio ya anga na silaha za ndege katika mji wa Ghouta Mashariki nchini humo.
Taarifa hii imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria ambalo liko nchini Uingereza ambalo limesema idadi hiyo ya vifo inahusisha watoto 58 na wanawake 42.
Shirika hilo limeeleza kuwa zaidi ya watu 1,200 wamejeruhiwa vibaya na mashumbulio hayo na kueleza kuwa takwimu hizo za vifo ni za juu zaidi tangu litokee shambulio la kemikali hapo hapo Ghouta Mashariki ambalo liliua takribani watu 1400.
Baba Mzazi wa Akwilina aomba kuonana na JPM, amesema ana siku 4 hajaoga
Ombi la Mbunge Rombo Selasini akiwa na Wazazi wa Akwilina, kwa Serikali