Leo February 21, 2018, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitalishtaki Jeshi la Polisi na Serikali endapo watashindwa kutoa tamko kuhusu watu 40 waliokamatwa siku ya maandamano katika uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika amesema watu hao 40 walikamatwa February 16, 2018 wakati wakielekea Manispaa ya Kinondoni.
Mnyika amesema hadi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia wananchi hao 40, ambapo kisheria lilipaswa kutoa haki kwa wananchi hao kupata dhamana.
“Tunalitaka jeshi la Polisi kupitia IGP kutoa kauli leo juu ya watu hao 40 wanaowashikilia na kuwaainisha kwa majina watu hao na kueleza taratibu za kuwapa dhamana ama iwapeleke Mahakamani.” – John Mnyika
“Hakikisheni upelelezi unakamilika, jamii inajua Mahakama ndio inachelewesha kesi” -Hakimu
Asasi za Kiraia “Ni kosa Polisi kujichunguza kwa Matukio yanayowahusu”