Kutoka Marekani Uongozi wa radio ya ‘The Arch’ iliyopo katika mji wa St Louis nchini humo kwa kushirikiana na hospitali ya St Louis imerusha matangazo ya moja kwa moja ya kujifungua kwa mtangazaji wake kutoka hospitalini.
Mtangazaji huyo ajulikanaye kama Cassiday Proctor ambaye anatangaza kipindi cha alfajiri kwenye siku za weekend, amekuwa akizungumzia ujauzito wake kwenye vipindi vyake vya radio na hivyo waliamua kufanya hivyo ili wasikilizaji wasikilize pia anavyojifungua.
Cassiday alishikwa na uchungu siku ya jumatatu ikiwa ni wiki mbili kabla ya muda aliotarajia kujifungua na akajifungua Jumanne February 20, 2018.
“Ilikuwa ni furaha sana kujifungua wakati niko hewani na wasikilizaji pia wanasikia, katika siku muhimu ya maisha yangu.” – Cassiday Proctor
Watu 8 wamekamatwa wakiwa Lita 4,000 za Gongo ndani ya Ziwa Victoria
Aliyekuwa Mgombea Ubunge Siha apanga kwenda Mahakamani kupinga Matokeo