Padre wa Parokia ya Yohana Mbatizaji, Kigogo Luhanga aliyeoongoza misa ya kumuombea Marehemu Akwilina Akwilini katika Viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Raymond Manyanga ameitaka Serikali kufanya uchunguzi kuhusu tukio la kupigwa risasi Marehemu Akwilina.
Akizungumza mbele ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa Padri Raymond amesema anayehusika kumpiga risasi binti huyo aliombe Taifa msamaha kutokana na kitendo hicho.
“Ndugu zangu sipendi kuingia ndani sana ya kwamba limetokeaje, huo sio uwanja wangu, mimi nizungumzie katika imani MUNGU anao ujumbe na tuufanyie kazi ili lisitokee tena, lakini aliyefanya aidha kwa nia nzuri au mbaya aliombe Tiafa msamaha,” -Padri Raymond
WANAWAKE WAZUNGUMZIA KUJISHUGHULISHA NA UVUVI WA PWEZA