Usiku wa February 22 2018 club ya Arsenal ilicheza game yake ya hatua ya 32 ya UEFA Europa League dhidi ya Ostersunds FK katika game iliyochezwa katika uwanja wa Emirates jijini London.
Arsenal pamoja na kuwa nyumbani lakini wamejikuta wakikutana na kipigo cha magoli 2-1, magoli ya Ostersunds FK yakifungwa na Hosam Aiesh dakika ya 22, Ken Nlata Sema dakika ya 23 wakati goli pekee la Arsenal lilifungwa na Sead Kolasinac dakika ya 47 ya mchezo.
Bahati imekuwa yao Arsenal na kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya Europa League kwa faida ya kufunga magoli mengi ugenini katika mchezo wa kwanza ambao ulimalizaka kwa Arsenal kupata ushindi wa 3-0 hivyo wanafuzu kwa aggregate ya jumla ya magoli 4-2.
Rais wa FIFA amemtaja Mbwana Samatta leo