Ni siku kadhaa sasa zimepita toka nahodha wa Azam FC Himid Mao awe nje ya uwanja kutokana na majeruhi na wote tukasikia kuwa Azam FC wamempeleka Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.
Taarifa ikufikie kuwa Himid Mao amesharudi Tanzania na afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga ametoa ripoti yake kuhusu maendeleo yake baada ya kutoka Afrika Kusini na kurudi Tanzania.
“Himid Mao ambaye alikwenda Afrika Kusini kwa matibabu yeye amesharejea lakini kama tulivyowaambia awali Himid Mao tutaendelea kumkosa uwanjani kwa takribani wiki tatu lakini amerudi na ripoti ya daktari wake ambayo amepatiwa kule Cape Town Afrika Kusini na atakuwa chini ya uangalizi wa daktari wa Azam FC”>>>Jafari Iddi
Rais wa FIFA amemtaja Mbwana Samatta leo