Leo Jumamosi February 24, 2018 kumekuwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha polisi Oysterbay, ambapo inasemekana wana majeraha ya risasi na mpaka sasa hawajapelekwa hospitali.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa watu hao wote watatu walijeruhiwa siku ya Ijumaa ya February 16, 2018 katika maandamano ya wafuasi wa CHADEMA kwenye kipindi cha uchaguzi mdogo, katika eneo la Kinondoni walipokuwa wakidhibitiwa na jeshi la polisi.
Hatahivyo Ayo TV na millardayo.com imefanya mawasiliano na Kamanda wa Polisi Kinondoni RPC Murilo Jumanne Muliro kuthibitisha suala hilo ambapo amesema ni kweli wanawashikilia watu hao lakini mtu yeyote akiwa mahabusu na kuhitaji matibabu, hupatiwa matibabu hayo kwa wakati.
Kamanda Murilo ameeleza kuwa mtuhumiwa yeyote akiwa mahabusu na akahitaji matibabu yoyote hata kama anaumwa malaria hupelekwa hospitali kutibiwa tena bila gharama yoyote hivyo hizo ni propaganda.
“Kuna Charge Room Officer ambaye moja kati ya kazi yake ni kuhakikisha kila baada ya masaa manne anakagua mahabusu kuangalia hali za watuhumiwa, kama kuna anayehitaji matibabu anapelekwa hospitali na hii haihitaji shinikizo ni haki yao kisheria na tumeshaifanya kabla wao hawajaongea.” – Kamanda Muliro
Wananchi waomba Jengo la Zahanati walilojenga kwa Fedha zao Wafugie Mifugo
Maamuzi ameyafanya Prof: Ndalichako kwa mtoto aliyekuwa analia kwenye msiba wa Akwilina