Club ya Mbao FC October 18 2017 ilipata bahati ya kupewa basi jipya na kampuni ya GF Trucks & Equipment na kuwa miongoni mwa club chache za soka Tanzania zinazomiliki mabasi yao wenyewe baada ya kutumia basi la kukodi kwa muda mrefu.
Baada ya Mbao FC kupewa basi hilo ilikuwa ni miongoni mwa club changa zenye usafiri wake ukizitoa club za Simba, Yanga, Azam FC, Mtibwa Sugar, Singida United na Mbeya City.
Kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba siku ya Jumatatu ya February 26, wachezaji wa Mbao FC kwa mara ya kwanza baada ya siku 130 wameamua kwenda kuwatembelea wadhamini wao GF Trucks na kuwashukuru kwa udhamini wao na kuwapatia basi jipya lenye thamani ya Tsh milioni 70.
Rais wa FIFA amemtaja Mbwana Samatta leo