Mashambulio mbalimbali ya kigaidi yanaendelea kutokea nchini Somalia ambapo usiku wa kuamkia leo February 24, 2018 watu 18 wameuawa baada ya shambulio la bomu katika mji wa Mogadishu.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetekelezwa na kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab karibu na Ikulu ya Rais wa nchi hiyo lakini hatahivyo maaskari walifanikiwa kuwaua kwa risasi magaidi watano ambao walihusika kwenye tukio hilo.
Mabomu hayo yalitegwa kwenye magari mawili ambapo moja lilienda kulipuka nje eneo la ikulu lakini jingine lililipuliwa mbele ya hoteli moja ambayo iko mbali kidogo na ikulu hiyo.
Viongozi wa kikundi hicho cha kigaidi walidai pia kuhusika katika shambulio lingine la milipuko ya mabomu na risasi katika mji mkuu huo ambalo liliua wanajeshi 15 mnamo September 15, 2018, lakini bado taarifa hii haijathibitishwa.
Wananchi waomba Jengo la Zahanati walilojenga kwa Fedha zao Wafugie Mifugo
Baada ya Wananchi kumkataa DC mbele ya Waziri Mkuu, Madiwani watoa msimamao wao