Siku za hivi karibuni nchi ya China imepiga hatua nyingine tena kwenye sekta yake ya elimu kwa kutambulisha michezo vya video (video games) kwenye mtaala wa shule.
Hii ina maana ya kwamba wanafunzi sio kwamba tu wataruhusiwa kucheza michezo hiyo wakiwa darasani, bali pia wanalazimika kusoma na kuicheza muda wowote wakiwa darasani au katika maeneo ya shule.
Kwa mujibu wa Kampuni ya Newzoo, mwaka 2018 sekta ya michezo ya kimtandao (eSports) inatarajiwa kuzalisha Dola za Marekani Milioni 906 sawa na Tsh Trilioni 2.1 katika mauzo duniani kote huku China ikichangia kwa asilimia 18 ya mauzo hayo.
Kampuni ya utafiti wa mtandao nchini China iReseach inaelezwa kuwa kwa sasa takribani watu Milioni 260 wanajihusisha katika kucheza michezo ya mtandao yaani eSport au mashindano ya kuangalia.
Siku 130 baada ya Mbao FC kukabidhiwa basi jipya
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi