Leo February 24, 2018 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezungumza na Balozi Dr. Wilbrod Slaa anayewakilisha Tanzania nchini Sweden pamoja na Muhidini Mboweto anayewakilisha nchini Nigeria ambapo amewataka mabalozi kutumia mbinu za kidiplomasia kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii na kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa nchini.
Waziri Mkuu amewataka mabalozi hayo wakaimarishe diplomasia kwa lengo la kuzifanya nchi hizo ziendelee kushirikiana na Tanzania katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Majaliwa amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kama uwepo wa fukwe za bahari kuanzia Tanga hadi Mtwara, maziwa na mito, mbuga za wanyama hivyo ni vema wakajielekeza katika kuvutia wawawekezaji kwenye sekta hiyo ili Taifa lipate watalii wengi.
Amesema mbali na kutangaza sekta ya utalii, pia watafute wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
“Tumejiimarisha katika mazao ya chakula na biashara, hivyo tunatakiwa kuwa na uhakika wa masoko kwenye kilimo ili mkulima anapozalisha pamba, tumbaku, kahawa, chai, korosho, dengu pamoja na mazao mengine tuwe na mahali pa kuuza, kwa hiyo washawishini wafanyabiashara kuja kununua.” -Waziri Mkuu Majaliwa
Waziri Mkuu amewasisitiza mabalozi hao kwenda kupunguza gharama za uendeshaji wa Balozi kwa kuzuia matumizi katika mambo yasiyo ya lazima. “Pia maslahi ya nchi lazima mkayasimamie huko muendako hasa katika masuala ya kiuchumi”
Kwa upande wao mabalozi hao wamesema watahakikisha wanayafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi wanazoziwakilisha.
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi