Baada ya alfajiri ya February 22 2018 Rais wa FIFA Giann Infantino na Rais wa CAF Ahmad Ahmad na viongozi wa nchi nyingine wanachama wa FIFA kutoka sehemu mbalimbali duniani kuwasili Tanzania kwa ajili ya mkutano wa FIFA wa maendeleo ya soka, Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe leo ameongea na waandishi wa habari.
Leo February 24 2018 Waziri Mwakyembe amefanya mkutano na waandishi wa habari na kuwapa taarifa wa kilichojadiliwa ndani ya kikao hicho kuhusiana na maendeleo ya soka na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinalikabili shirikisho la soka Tanzania TFF.
Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa FIFA ilikata kutoa pesa kwa TFF muda mrefu lakini baada ya shikisho hilo kujisafisha sasa watakuwa wanapata pesa kama kawaida lakini good news ni kuwa FIFA wameongeza pesa kwa nchini wanachama kama Tanzania sasa itakuwa inapewa dola milioni 1.25 kutoka kupewa dola 250000 kwa mwaka.
Rais wa FIFA amemtaja Mbwana Samatta leo