Leo February 24, 2018 Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ameomba kuwepo kwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano ya kisiasa kutokana na kuwepo kwa vitendo vya kupigwa, kuumizwa, kuuwawa pamoja na kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa Pamoja na hayo amezungumzia suala la yeye kukamatwa na polisi kwa madai yakufanya mikutano bila kibali.
“Hizi ni dalili mbaya sana, haya yanaashiria Watawala wa sasa hawataki Mfumo wa Vyama Vingi, tunataka uitwe Mkutano wa Kitaifa wa maridhiano ya kisiasa, ili Watawala waongee yanayowakera na Sisi tuwaambie Watawala yanayotukera” -Zitto Kabwe
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi