Leo February 25, 2018 Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi amezungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto mbalimbali zinazozuia wanawake kushiriki katika nafasi za Uongozi nchini na jinsi ya kuweza kutoka katika changamoto hizo.
Liliana amesema TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wengine wanaotetea haki za wanawake na usawa wa jinsia wameaanda kongomanao la Wanawake na Uongozi ili kutoa fursa kwa Wanawake na wadau wengine kutafakari na kupanga mikakati ya kuimarisha ushiriki wa Wanawake katika Uongozi.
Lilian ametaja baadhi ya vitu vinavyosababisha Wanawake kushindwa kushiriki kikamilifu katika nafasi za kuongoza kuwa ni ukosefu wa elimu, mimba za utotoni huku wanawake wengine wamekuwa wakitumia Saa 10 hadi 15 kufanya kazi za huduma katika familia
“Pamoja na juhudi zote, wanawake bado wanakumbana na vikwazo mbalimbali vinavyokwamisha kushiriki kikamilifu katika nafasi na fursa za kuongoza, vikwazo hivyo ni ukosefu wa fursa za elimu, mimba za utotoni, ukatili wa kijinsia na ukosefu wa fursa za kumiliki ardhi,” -Lilian Liundi
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi