Leo February 26, 2018 Baada Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kumhukumu Miezi Mitano jela Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amesema hukumu ya leo sio mwisho wa mjadala Mahakamani na kwamba bado kuna fursa na haki ya rufaa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani.
“Pili, hukumu ya leo haina maana Sugu atakaa gerezani muda wote huo. Kuna haki ya dhamana pending appeal. Ndivyo ambavyo tumefanya kwa viongozi na wanachama wetu wengi in the past.” -Tundu Lissu
“Tatu, hukumu ya leo haina athari yoyote kwa Ubunge wa Sugu. Katiba inaweka masharti ya kifungo cha miezi sita au zaidi na kwa makosa ya ‘utovu wa uaminifu’ uchochezi au kutoa lugha ya matusi sio makosa ya utovu wa uaminifu.” -Tundu Lissu
BREAKING: ‘SUGU’ ALIVYOFIKA MAHAKAMANI, UKAGUZI ULIOPO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
MAHAKAMANI: ‘WEMA KANIAMBIA ANAVUTA BANGI KWA STAREHE’ -POLISI, BONYEZA PLA HAPA CHINI KUTAZAMA