February 26 2018 Mbeya Tanzania hukumu ya miezi mitano jela imetolewa kwa Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi pamoja na Emmanuel Masonga ambae ni Katibu wa CHADEMA Kanda za juu kusini kwa kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.
Wake za Viongozi hao wameongea na Waandishi wa Habari kuhusu hukumu hiyo ambapo Mke wa Sugu Happyness Msonga “hukumu ni hukumu tu hauwezi kuifurahia hata kama ingekua ni wiki moja, Joseph ni Mpambanaji siku zote, ni Sugu Sugu tu hata leo nimetoka kuongea nae he is okey“
Grace ambae ni Mke wa Masonga amesema “Hakimu ametoa hukumu lakini tumekata Rufaa kwahiyo tunasubiri tuone mchakato utakavyokua, kuna vitu ambavyo tumezoea kuvifanya pamoja katika kujenga familia sasa naona kama vile kuna baadhi ya mambo itabidi yasimame kwa muda“
Unaweza kuwatazama wakiongeza zaidi kwenye hii video hapa chini
MATANO ALIYOSEMA WAKILI PETER KIBATALA KUHUSU RUFAA YA SUGU
FULL VIDEO: SUGU NA MASONGA WAKIPELEKWA GEREZANI… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA