Wakili Peter Kibatala anaemtetea Mbunge Joseph Mbilinyi pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emmanuel Masonga waliohukumiwa kwenda jela miezi mitano Mbeya February 26 2018 amezungumza hatua lilipofikia suala la Rufaa katika kesi hiyo.
“Hatujaharidhika na maamuzi tumefuata taratibu kadhaa za kisheria kwa watu ambao hawajaridhika na maamuzi ya Mahakama, tumetoa taarifa ya kukata Rufaa, tumeleta maombi ya dhamana, tumeomba Mahakama itupe nakala za mwenendo wa kesi kwa sababu ni kitu muhimu katika kukata rufaa,” -Peter Kibatala
FULL VIDEO: SUGU NA MASONGA WAKIPELEKWA GEREZANI… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA